Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yakiri kusuasua biashara ya Almasi

Almasi Tanzania Biashara Serikali yakiri kusuasua biashara ya Almasi

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

“Kwa kipindi cha kuanzia Julai 2023 hadi Machi 2024, bei ya madini ya dhahabu kwa wakia ilipanda hadi kufikia wastani wa Dola za Marekani 2,138.01 ikilinganishwa na bei ya wastani wa Dola za Marekani 1,854.54 katika kipindi cha Julai 2022 hadi Machi 2023.

Kuongezeka kwa bei ya dhahabu kunatokana na sababu mbalimbali ikiwamo mahitaji makubwa ya madini hayo duniani, Mheshimiwa Spika (Dkt. Tulia Ackson) kwa upande wa madini ya almasi katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, mwenendo wa biashara ya madini hayo duniani umeendelea kusuasua kutokana na mdororo wa uchumi uliosababishwa na madhara ya vita kati ya Urusi na Ukraine. Madini hayo yameshuka bei duniani kwa asilimia 19 kwa mwezi Machi, 2024”- Mavunde.

Waziri wa Madini Anthony Peter Mavunde akiwasilisha bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, siku ya Jumanne Aprili 30, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live