Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yakaribisha sekta binafsi kuwekeza viwanda 10

759b3ea35a9c22c466477bb7454874aa Serikali yakaribisha sekata binafsi kuwekeza viwanda 10

Mon, 23 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imefungua milango kwa sekta binafsi kuwekeza katika viwanda 10 kati ya 20 ilivyovirejesha baada ya wawekezaji wa awali kushindwa kuviendeleza kwa mujibu wa masharti ya kubinafsisha viwanda hivyo.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo ametangaza Jijini Dar es Salaam Agosti 23 kuwa viwanda vingine vinane vimekabidhiwa kwa Mamlaka ya Uzalishaji wa Mauzo ya Nje (EPZA) kwa ajili ya uwekezaji kwenye maeneo maalum ya kiuchumi (SEZ).

Hata hivyo amesema viwanda viwili vilivyosalia vitakabidhiwa kwa mashirika ya umma ili waviendeleze kwa kuingia ubia na wawekezaji wa sekta binafsi. Viwanda hivyo ni Mang’ula Mechanical Machine Tools kilichopo Morogoro ambacho kitakabidhiwa kwa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na kiwanda cha Mbeya Ceramics Co. Ltd kitakacho kabidhiwa kwa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO).

Aidha alisema viwanda vinane vilivyokabidhiwa kwa Mamlaka ya Uzalishaji wa Mauzo ya Nje (EPZA) kuwa ni kiwanda cha Mwanza Tanneries, Mwanza, TPL Shinyanga Meat Plant, Mafuta Ilulu, Lindi, Nachingwea Cashew nut na Mkata Samwill Limited kilichopo Tanga.

Viwanda vingine ni TPL mkoani Mbeya, Sikh Samwill Limited, Tanga na National Steel Corporation kilichopo Dar es Salaam.

Katika Miaka ya 1990, Serikali ilibinafisisha viwanda 156 lakini katika tathimini yam waka 2017 ilibaini viwanda 88 pekee vilikuwa vinafanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya mikataba husika. Viwanda 68 vilikuwa havifanyi kazi kwa mujibu wa mikataba na kati ya hivyo viwanda 20 vilikuwa vimepoteza sifa ya kuwa viwanda.

Chanzo: www.habarileo.co.tz