Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yakanusha kudaiwa na Benki ya Ulaya

Eib.jpeg Serikali yakanusha kudaiwa na Benki ya Ulaya

Sun, 5 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAARIFA YA SERIKALI

Kuna taarifa inasambaa mitandaoni ikidai kuwa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya EIB, inaidai Tanzania dola za Kimarekani bilioni 4.1 (zaidi ya shilingi trilioni 10 za Kitanzania) na kwamba mwezi Januari, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, aliomba mkopo mwingine kwenye Benki hiyo, lakini ilikataa kutoa mkopo huo kwa sababu haijalipwa deni kwa muda wa miezi 28.

Mara kwa mara, Mtandao wa kijamii wa Tanzania Abroad TV (TAT), umekuwa ukitoa taarifa za uzushi, upotoshaji na uzandiki dhidi ya Wizara ya Fedha na Mipango na Serikali kwa ujumla huku lengo lake likiwa halifahamiki bayana.

Tunawaomba Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa, mzipuuze taarifa hizo, ambazo hazina ukweli wowote na kwa vyovyote vile zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki isiyokuwa na sababu za msingi.

Pamoja na kwamba EIB ni mdau mkubwa wa maendeleo na ina uhusiano mzuri na nchi yetu pamoja na Sekta binafsi kwa muda mrefu na ina uhusiano mzuri na nchi yetu kwa ujumla, Serikali haina mkopo wa kiasi hicho kilichotajwa kutoka katika Benki hiyo.

Tunapenda kuwakumbusha wamiliki na watoa habari katika mitandao ya kijamii kwamba ni kosa kisheria kutoa taarifa za upotoshaji, uzandiki na uzushi kwa mujibu wa Sheria ya Huduma ya vyombo vya Habari (2016).

Hivyo tunatoa onyo kwa mtandao wa kijamii wa TAT na watu wengine wanaoeneza taarifa za namna hiyo mitandaoni kuhusu Wizara ya Fedha na Mipango, na kuchafua tawira nzuri ya Wizara na Serikali katka jamii, kuacha tabia hiyo mara moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live