Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yakamilisha uwekezaji gesi asilia

Serikali Yakamilisha Uwekezaji Gesi Asilia Serikali yakamilisha uwekezaji gesi asilia

Wed, 5 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema imefikia hatua za mwisho za mazungumzo na mwekezaji atayewekeza katika mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia kuwa kimiminika.

Imesema baada ya mazungumzo hayo itasaini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya Sh trilioni 70 utakaofanywa na kampuni za Shell ya Uholanzi na Equinor ya Norway.

Akizungumza katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere maarufu Sabasaba, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba amesema hatua hiyo ni njema kwani dunia imehamia kwenye nishati rafiki ya gesi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live