Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yakamilisha ujenzi majosho 7 Msomera

Majosho Sababaa Serikali yakamilisha ujenzi majosho 7 Msomera

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI imekamilisha ujenzi wa majosho saba kwa ajili ya kuoshea mifugo, miradi kwa ajili ya malisho ya mifugo ambapo maandalizi yamekamilika yakiwemo ya upatikanaji wa mbegu.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema kwa mwaka wa fedha 2023, serikali imetenga fedha Sh Bilioni 5.9 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji kwa wafugaji, ikiwemo kujenga minada mkwa ajili ya kujenga minada mipya, kukarabati ya zamani na kutengeneza majosho.

“Namshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo serikali yake inahakikisha kila sekta inafikiwa katika maendeleo wakiwemo wafugaji na wavuvi,” amesema.

Ulega amebainisha hayo wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Kijiji cha Msomera kilichopo Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayowahusu wafugaji, yakiwemo mabwawa ya maji, minada ya mifugo, majosho na malambo ili kusogeza huduma karibu kwa wakazi wa kijiji hicho.

Amesema mbali na wafugaji ambao serikali imekuwa ikiwafikia kwa kuwapatia huduma mbalimbali za miundombinu kwa ajili ya shughuli za mifugo, wavuvi na wafugaji wa samaki pia wanafikiwa.

“Hakuna mradi uliosimama yote inasonga mbele makandarasi waendelee kushirikisha vyema wenyeji ambao wanajua mazingira ya hapa na wenyeji kushirikiana na makandarasi na wenyewe kuwashirikisha viongozi kila hatua,” amesema Ulega.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Albert Msando akitoa taarifa ya wilaya kwenye kikao cha Kijiji cha Msomera, ambacho Naibu Waziri Ulega alikuwa mgeni rasmi, amesema hadi sasa serikali imeshajenga majosho saba kwa ajili ya kuoshea mifugo, miradi kwa ajili ya malisho ya mifugo ambapo maandalizi yamekamilika yakiwemo ya upatikanaji wa mbegu.

Msando ameongeza kuwa idadi ya mifugo iliyopo katika kijiji hicho ni mingi kuliko idadi ya wakazi wake, ambapo inafikia zaidi ya 86,234 ikiwemo ng’ombe 28,049 mbuzi 32,743 kondoo 24,795 na punda 647.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live