Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yajipanga kushusha bei vifurushi vya intaneti

TCRA Mabandooo.png Serikali yajipanga kushusha bei vifurushi vya intaneti

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye @napennauye ametoa ufafanuzi kwa waliouliza maswali ya data kwa nia ya kuelewa na kujadiliana kwa staha kwa lengo la kupata muafaka ambapo amesema “Kwamba Rais Samia hajachukua hatua juu ya jambo hili si kweli, bei ya juu Mwezi 3/2021 ilikuwa Tsh. 40.04, bei ya juu Mwezi 8/2022 ni Tsh. 9.35”

“Tuanzie hapa na ukisoma majedwali haya mawili (kwenye swipe) utaona kuwa kazi ya kwanza ya Serikali ya awamu ya sita ilikuwa kutoa bei ya juu ilikokuwa imefika yaani Tsh. 40.4 kurudi mpaka Tsh. 9.35, inawezekana kwa wengine hili si jambo kubwa lakini ni kweli si jambo kubwa?”

“Vifurushi ambavyo mara zote nimesema ni huduma ya ziada ambayo kwa Tanzania imegeuzwa kuwa huduma ya msingi mwezi 03/2021 ilikuwa Tsh. 1.11 mpaka 2.80 na baada ya kutengeneza msawazisho wa kupunguza ya juu ndio tukapata wastani wa Tsh. 1.75 mpaka Tsh. 4.67, sasa kama ulivyo uzalishaji wa bidhaa zingine zozote kuna gharama za kuzalisha unit moja inayosafirisha data”

“Serikali inaendelea kuona namna gani tutapunguza gharama za kuzalisha data nchini ili bei yake ishuke, kazi ya kwanza ilikuwa kupata uhalisia wa bei ya data halafu ndio unaagalia kitu gani kinaweza kufanywa ili kupunguza gharama za uzalishaji ili kusaidia kupunguza bei ya Data. Ndio kazi serikali tunaendelea nayo tuone maeneo gani yakiguswa yatapunguza bei ya kuzalisha”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live