Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaitoa hofu sekta binafsi

C780e5a35ac48e831589452f9440db9d Serikali yaitoa hofu sekta binafsi

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI imesema itahakikisha inaendeleza mahusiano mazuri na sekta binafsi, kwa kuandaa mazingira mazuri ya kuwa pamoja ili kufanya kazi pamoja ambayo itakuwa na tija kwa taifa.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki na kuzitaka sekta binafsi ambazo zinahusika na masuala ya chanjo kutokua na shaka.

“Tuliona kasoro, lakini niwaombeni sekta binafsi hasa wale mlio vizuri katika jambo hili la chanjo msiwe na wasiwasi hata mkiingia mikataba na halmashauri ili mradi muwe na sifa na vigezo ndiyo maana ya sisi tukatoa mwongozo ili tufanye kazi pamoja.” amesema Waziri Ndaki saa chache baada ya serikali kutoa muongozo wa utoaji chanjo kwa wagonjwa.

Pia, amewataka viongozi wenzake wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mamlaka za Serikali za Mitaa, watoa huduma za afya ya mifugo na Sekretarieti za Mikoa wazingatie maelekezo yaliyopo kwenye mwongozo wa utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo nchini na kutoa maoni au kuuliza maswali sehemu ambazo zitakuwa na utata ili kuhakikisha mwongozo huo unatekelezwa kama ambavyo umezingatiwa kwa ajili ya kudhibiti magonjwa ya mifugo nchini.

Ameitaka pia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoa nakala za kutosha za mwongozo huo kwa wadau wa sekta ya mifugo kote nchini na pia kuwataka wadau kupata nakala laini kupitia tovuti ya wizara hiyo,

Chanzo: habarileo.co.tz