Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi waje kuwekeza kwenye kilimo cha chikichi kwa kuwa nchi ina ardhi ya kutosha na yenye rutuba.
Majaliwa alitoa wito huo jana bungeni Dodoma wakati akijibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Assa Makanika (CCM).
Katika swali lake, Makanika alisema nchi inapitia wakati mgumu wa kuagiza mafuta ya kula nje kwa ajili ya kujaza nakisi ya lita 250,000 hadi 300,000 na kutumia Sh bilioni 480, hivyo alitaka kujua serikali ina mkakati gani wa kupunguza nakisi hiyo.
“Ardhi tunayo na tumeshatoa maagizo kwa wakuu wa mikoa wote kutenga ardhi kwa ajili ya uwekezaji,” alisema Majaliwa. Aliongeza: “Tunataka tuzalishe na tukamue mafuta yetu sisi wenyewe, tunaamini gharama itakuwa ndogo na zile fedha tunazotumia kuagiza mafuta nje hazitakwenda tena bali tutaziingiza kwenye shughuli nyingine za kimaendeleo.
Uwekezaji huu ni mkubwa na endelevu.” “Sasa tunakwenda kuimarisha viwanda vya ukamuaji ili tuweze kukamua asilimia 99 ya mafuta kwenye chikichi badala ya 70 ya sasa,” alisema.
Alisema serikali inatoa mwito kwa wawekezaji kwenda kuwekeza Kigoma, Mpanda, Katavi na hata Sumbawanga kwani kuna maeneo ya kutosha kuendesha kilimo cha chikichi, kukamua na kupata mafuta yenye gharama ndogo na hivyo kupunguza kiwango cha fedha kwenda kununua mafuta ya kupikia nje.
Wakati huoho, Majaliwa amesema serikali imetoa vibali kwa wawekezaji kuingia katika uwekezaji wa usafirishaji mifugo na mazao yaliyoboreshwa ili kupata tija.
Alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Azan Mwinyi aliyetaka kufahamu serikali inaweka mkakati gani kuimarisha usafirishaji wa mifugo na mazao katika nchi za Kenya, Madagascar na Comoro ili wafanyab