Serikali imengiza Sh milioni 68 kuanzia Julai, 2022 hadi Februari, 2023 badaa ya watalii zaidi ya 12,000 kutembelea Hifadhi ya Msitu Ziwa Duluti uliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Mhifadhi mwandamizi wa msitu huo ambao uko chini ya Wakala wa Msitu Nchini {TFS}, Peter Myonga amesema watalii hao 10,000 ni kutoka ndani na 2,000 nje ya nchi. Amesema hayo wakati akieleza mpango kazi wa TFS katika miaka ijayo ambapo amesema kuwa lengo ni kuboresha na kuingiza kipato zaidi kwa serikali.
Myonga amesema katika Watalii wa nje ambao wengi wao walivutiwa na filamu ya Royal Tour iliyoandaliwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan iliyoangalia sehemu nyingi Duniani walivutiwa na vivutio kadhaa Nchini ikiwemo Ziwa Duluti na kuamua kwenda kutembelea ziwa hilo lenye historia ya kuwa na Kenge wengi na Utalii wa picha kuliko ziwa lolote Nchini.
Alisema Ziwa Duluti lilianzishwa mwaka 1965 lenye ikolojia yenye mimea zaidi ya 350,ndege 500.kenge 700 na lina sifa ya kuwa na maji kwa muda wote yenye utulivu bila ya kukauka.
Mhifadhi huyo alisema kuwa kwa sasa TFS imetangaza fursa kwa wawekezaji wa Lodge na Mgahawa wa ndani na Nje kwenda kuwekeza katika Hifadhi ya Ziwa Duluti ili wageni watapokwenda kutembelea Hifadfhi hiyo waweze kupata huduma hizo kwa haraka na upesi.
Myonga alisema Hifadhi ya Msitu wa Ziwa Duluti mbali ya kuwa na Msitu Mnene wenye utulivu mkubwa pia eneo hilo la Ziwa Duluti limejaliwa kuwa Utalii wa picha na Utalii wa samaki na hivyo ni vivutio tosha kwa Watalii wa Nje na ndani.
‘’TFS inahamasishisha Wawekezaji wa Ndani na Nje kuja kuwekeza katika Hifadhi ya Ziwa Duluti hususani Uwekezaji wa Lodge na Mgahawa kwa ni eneo maalumu kwa mapumziko kwa wageni wa aina yoyote’’alisema Myonga
Naye Mwekezaji wa Mgawahawa wa Chakula raia wa Nchini Israel,Alex Vaknin na Mke wake Victoria Petrovsky wamesema kuwa uwekezaji waMgahawa katika eneo la Ziwa Duluti ni uwekezaji waliokuwa wakiutafuta kwa muda mrefu na ana uhakika kuwa utamlipa.
Waisrael hao walitoa wito kwa wawekezaji wengini wa Lodge na Mgahawa kwenda kuwekeza Duluti kwani kuna sifa zilizotukuka katika Utalii wa Picha na Majini.
‘’Eneo hili ni zuri na nilikuwa kila siku nikitamani eneo kama hili kuwekeza Uwekezaji wa Mgahawa sasa nimefanikiwa kupata naisifu serikali ya Rais Samia kwa kuvutia wawekezaji wa Utalii na ntakuwa nanipa vyakula hata vya nyumbani kwetu’’alisema
Naye Mfanyabiashara wa Utalii Mkoani Arusha,Daud Lusewa alisema kuwa eneo la Ziwa Duluti linapaswa kutangazwa kwa nguvu zote kwani ni eneo maalumu lenye sifa za utulivu na Utalii wenye kuvutia hivyo serikali inapaswa kutumia nguvu kubwa kulitangaza ziwa hilo.
Lusewa alisema Mkoa wa Arusha una maeneo machache sana yenye sifa ya Ziwa Duluti hivyo ni wajibu wa Mkoa na TFS kuhakikisha uwekezaji wa Lodge na Mgahawa unafanyika ili kurahishisha huduma kwa wageni.