Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaingilia kati sakata la sukari kupanda bei

Sukari2 Serikali yaingilia kati sakata la sukari kupanda bei

Wed, 3 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imetoa vibali kwa wafanyabiashara kuagiza tani 50,000 za sukari kutoka nje ya nchi, ikiwa ni hatua ya kunusuru kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo nchini.

Hatua hiyo ya Serikali imetokana na ongezeko la bei na uhaba wa bidhaa hiyo katika mikoa mbalimbali, ikiwamo Manyara ambako kilo moja inauzwa Sh4,000 kutoka Sh3,000.

Hali ni mbaya zaidi katika Mkoa wa Arusha, bei ya kilo moja ya sukari imeongezeka kutoka Sh3,000 hadi Sh4,500 na Sh5,000.

Kwa upande wa Mkoa wa Kilimanjaro, kilo moja ya bidhaa hiyo kwa sasa inauzwa kwa Sh3,800 kutoka Sh3,000 ya awali.

Hata hivyo, wazalishaji wa sukari wamesema kupungua kwa uzalishaji wa bidhaa hiyo viwandani, kumesababishwa na mvua za El-Nino.

Akizungumza na Mwananchi jana, Januari 2, 2024 Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari (SBT), Profesa Kenneth Bengesi amesema kilichotokea si uhaba, ni dharura ya kupungua kwa uzalishaji viwandani.

“Mvua ina athari kubwa kwenye uzalishaji wa sukari kwa sababu mashamba ya miwa mengi yapo mabondeni, ikinyesha mvua kubwa miwa inanyonya na inapunguza sukari,” amesema Profesa Bengesi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live