Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yafungua mnada wa kimataifa wa mifugo Longido

Sat, 22 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Longido. Serikali ya Tanzania imezindua mnada wa kimataifa wa mifugo wilayani Longido mkoani Arusha huku ikiwaonya wafugaji kuacha mara moja tabia ya kuvusha mifugo kwenda kuuza nchi jirani ya Kenya kinyemela.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mnada huo, Mkuu wa mkoa Arusha, Mrisho Gambo amesema Serikali imezindua mnada huo ili kudhibiti tabia ya utoroshwaji mifugo, kuondoa urasimu na kulinda maslahi ya wafugaji.

Amesema Serikali imetumia Sh932.7 milioni kujenga mnada huo hivyo ni lazima wafugaji  kutumia kwa kuuza na kununua mifugo na wanunuzi wa nchi jirani ya mifugo wanapaswa kufika katika mnada huo kununua mifugo.

Katibu Mkuu wizara ya mifugo na Uvuvi,  Profesa Elisante Ole Gabriel amesema mnada huo wa kisasa unapaswa kutumika kuuza na kununua mifugo na sio njia tu ya kulipia ushuru.

Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe amesema serikali wilaya ya Longido, imejipanga kuhakikisha eneo hilo la mnada linatumika vizuri na imepangwa kila Jumatano uwepo mnada mkubwa na siku nyingine zote za wiki kuwe na biashara za mifugo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Longido, Jumaa Mhina amesema wilaya ya Longido utajiri wake mkubwa ni mifugo kwani ina ng'ombe217,293, mbuzi 399,754,kondoo 301,211 na punda 15,339.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz