Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yafungua fursa uwekezaji nishati

Ewura Makamba Pic Waziri wa Nishati, January Makamba

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema moja ya chnagamoto kubwa katika sekta ya umeme nchini ni uwekezaji usiojitosheleza katika sekta hiyo na kuwa kwa kipindi chamwaka mmoja wa Rais Samia ameweza kuifungua nchi katika fursa za uwekezaji.

Vile vile, Waziri Makamba amesema lengo ni kurudisha imani kwa nchi tajiri na wawekezaji wakubwa kuja kuwekeza Tanzania na kufungua milango uwekezaji kwenye nishati.

Waziri Makamba, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza kwenye kipindi cha “Kwa Maslahi ya Taifa.” Alisema: “Kwa nchi yenye ukubwa kama wa nchi yetu, na inayokuwa kwa kasi kama yetu, na ongezeko la idadi ya watu, hadi kufikia watu milioni 60, kuwa na Megawati 1,600 ni aibu kubwa, au kuwa na mtandao mdogo wa usafirishaji umeme kama tulionao ni aibu.”

Akizungumzia mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani, alisema ni pamoja na kuendelea kuifungua nchi kwa wawekezaji wakubwa na kutolea mfano, kwenye Kongamano la Uwekezaji Sekta ya Nishati, lililofanyika Siku ya Tanzania, kwenye Maonyesho ya Expo Dubai, na kuhudhuriwa na Rais Samia.

“Ttumezungumza na wawekezaji wengi, wakubwa wenye uwezo, na nia njema ambao wako tayari kuja nchini kwetu na kuwekeza katika maeneo hayo,” alisema.

Alisema uwapo wa Rais Samia kwenye kongamano hilo, umeleta hamasa ya kipekee kwa kuvutia wawekezaji wakubwa kuhudhuria na kuendelea kufungua milango ya fursa za uwekezaji mkubwa kwa Tanzania.

Kuhusu mafanikio kwenye sekta ya nishati, alisema ni pamoja maendeleo ya mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) wa kuzalisha umeme, kwenye Stigler Gorge, toka mradi huo umeanza, limejengwa bwawa pekee la kuzalisha umeme, lakini baada ya Rais Samia kuingia, ametoa fedha za ujenzi wa miundombinu ya kuusambaza umeme unaozalishwa, ili ufike kwenye Gridi ya Taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live