Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yafafanua mikopo benki ya kilimo

575433226529331a440f43789b25df2e Serikali yafafanua mikopo benki ya kilimo

Wed, 21 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu tathmini ya mikopo inayotozwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kuwa ni kwa ajili ya kulipia gharama za uchambuzi wa maombi ya mkopo ambayo inahusisha shajala, uhakiki wa mradi na dhamana ya mkopo.

Ufafanuzi huo umetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba mapema leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee lililohoji ‘sababu Serikali kuweka tozo ya ada ya tathmini ya asilimia moja kwa mkopaji ambapo asilimia 50 inalipwa kabla ya kuanza kufanya tathmini na asilimia 50 inalipwa baada ya mkopo kuidhinishwa.

Akijibu swali la pili kuhusu kigezo kinachotumika tozo kuwa asilimia moja, Waziri Nchemba amesema kuwa kigezo kinachotumika kutoza ada ya uchambuzi wa maombi ya mikopo ni gharama halisi za uchambuzi wa maombi ya mkopo zinazotokana na nguvu ya soko kwa wakati husika.

Amesema kuwa utaratibu huo ni wa kawaida kwa taasisi za fedha kutoza ada ya uchambuzi wa maombi ya mikopo.

Aidha, ameongeza kuwa endapo mkopo hautaidhinishwa, asilimia 50 ya asilimia moja iliyolipwa haitarejeshwa kwa mwombaji wa mkopo kwa kuwa kiasi hicho kimetumika kulipa gharama za uchambuzi wa mkopo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz