Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yafafanua matumizi ya bil 52/-

6900 PHILIP MPANGO New TZW

Mon, 23 Apr 2018 Chanzo: habarileo.co.tz

SHILINGI bilioni 51.8 zililipwa na Serikali kununulia ndege aina ya Q 400 Bombadier iliyoingia nchini Aprili 2, mwakia huu, kuimarisha usafiri wa ndege nchini.

Imebainishwa kuwa ununuzi wa ndege hiyo ni sehemu ya Sh bilioni 52.67 ambazo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alizionesha katika ripoti yake kwamba zililipwa lakini vifaa havikupokelewa.

Akitoa ufafanuzi kuhusu fedha hizo mwishoni mwa wiki, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philipo Mpango alisema fedha hizo za mashirika manane ya Serikali Kuu zinaonekana zilitolewa lakini ukweli zilitumika kununulia ndege hiyo.

Dk Mpango alisema ni kweli CAG katika ripoti aliyowasilisha bungeni Aprili 11, mwaka huu na kuzungumza na vyombo vya habari inaonesha Sh bilioni 52.67 ni manunuzi ya vifaa na huduma ambazo ziliingia nchini baada ya kulipiwa lakini havikupokelewa.

Mkaguzi alisema ofisi yake ilibaini kwamba kuna manunuzi ya vifaa, kazi na huduma zenye thamani za fedha hizo ambazo zililipwa lakini vifaa vyake havikupokelewa.

"Ukaguzi katika taasisi za serikali nane ulibaini manunuzi ya vifaa, kazi na huduma zenye thamani ya Sh bilioni 52.67 vilivyoagizwa na kulipiwa havikupokelewa," alisema CAG katika ripoti yake.

Mkaguzi mkuu alionesha kwamba taasisi nane za serikali kuu zilinunua vifaa na huduma zenye thamani ya fedha hizo ambavyo viliingizwa nchini na kulipiwa lakini havikupokelewa.

Ukweli ni kwamba fedha hizo zimetumika katika kununulia ndege hiyo yenye kubeba abiria 75 imeingia nchini mapema mwezi huu kwa ajili ya kuongeza na kuboresha usafiri wa anga.

Fedha hizo zilitumika katika kununulila ndege mpya ya Shirika la Ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Aprili 2, 2018 ambayo Rais John Pombe Magufuli aliishuhudia ikimwagiwa maji wakati inaingia katika uwanja mara baada ya kuwasili kutoka Canada.

Chanzo: habarileo.co.tz