Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yafafanua kuhusu mikopo asilimia 10

Fedhapic Serikali yafafanua kuhusu mikopo asilimia 10

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Deogratius Ndejembi amesema kuwa ripoti ya maboresho ya mikopo ya asilimia kumi imefikishwa kwa Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Ndejembi ameyasema hayo leo Februari 2 wakati akijibu maswali ya wabunge ambapo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mwantumu Zodo aliyetaka kujua ni lini serikali itarejesha mikopo hiyo ili kuondoa adha ya mitaji wanayopata wanawake nchini hususan Mkoa wa Tanga.

Naibu Waziri Ndejembi amesema kuwa mikopo hiyo ilisitishwa baada ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuonyesha fedha nyingi za mikopo hiyo haijarejeshwa na Waziri wa TAMISEMI kuunda timu iliyopitia mikopo hiyo inavyotolewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live