Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji

Kunenge Pic Data Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema Serikali inaendelea kujenga na kuboresha mazingira bora ya wawekezaji ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora na zitakazoweza kushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Kunenge amesema hayo akijibu changamoto zilizowasilishwa na baadhi ya wawekezaji wa viwanda wilayani Bagamoyo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua shughuli zinazoendeshwa katika viwandani hivyo.

"Niwahakikishie wawekezaji endeleeni kuwekeza, umeme wa kutosha upo , na nasema hivi kwa sababu Rais wetu Samia Suluhu ametuahidi kuziondoa na ameanza kwa mradi huu wa Nyerere Hydropower Project huko Rufiji ambao umeme wake utazalishwa hapo na utatumika ukitokea hapa Chalinze inapojengwa mradi huo” amesema Kunenge

Kuhusu maji, mkuu huyo wa mkoa ameeleza Serikali imesaini mkataba na mkandarasi anafanya upembuzi yakinifu kutoa maji kutoka bwawa la mto Rufiji utakao zalisha lita milioni 250 kwa siku yatakayotumika Pwani na Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live