Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yadhibiti uchakachuaji sekta ya mafuta

Mafuta Mjadala Serikali yadhibiti uchakachuaji sekta ya mafuta

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kupitia Wakala wake wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja (PBPA), imeeleza kujitokeza kwa Changamoto kadhaa hususani baada ya Biashara ya Mafuta kufanyika huria kutokana na Mabadiliko ya Sera, ambapo hali hiyo imesababisha Kampuni za Mafuta Kuuza Nishati hiyo kwa Bei ya Juu kwa Kisingizio cha Kupanda kwa gharama kwenye Soko la Dunia.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa PBPA Erasto Simon wakati akitoa Wasilisho la Utekelezaji wa Majukumu ya Wakala huo na Mafanikio yake kwenye kikao kazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

"Pamoja na ongezeko la uwekezaji kwenye Sekta hii ya mafuta lililotokana na Sera ya Biashara huria, Changamoto kadhaa ziliendelea kujitokeza ikiwemo ile ya kuibuka kwa Wimbi la Uwekezaji ulio chini ya kiwango kwenye miundombinu ya mafuta kwenye mkondo wa Chini" amesema Erasto.

Kuhusu hatua mbalimbali zilizo chukuliwa na PBPA kwa ajili ya kukabiliana na Changamoto hizo na kuokoa kiasi cha Bilioni 500 tangu kuanzishwa kwa Wakala huo, Erasto amesema Serikali ilianzisha Mifumo mbalimbali ili kuhakikisha Changamoto zote zinamalizika.

"Utatuzi wa Changamoto zilizojitokeza baada ya kuanza kwa Soko huria kwenye biashara ya mafuta ni kuanzishwa mifumo mbalimbali ikiwemo kutungwa kwa Sheria ya Petroli, upangwaji wa bei ya mafuta, kuanzishwa kwa Mfumo wa Uagizaji wa mafuta kwa pamoja" amefafanua Erasto.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji huyo wa PBPA, amesisitiza kuwa Wakala huo utaendelea kuboresha mfumo wa uagizaji mafuta kwa Pamoja (BPS), ili kupata Bei halisi katika Soko la Dunia, ikiwemo kuongeza kiwango cha mafuta nchini.

"Kwa sasa Tanzania ina maghala 22 yenye uwezo wa kupokea mafuta kutoka kwenye meli baharini, maghala hayo yana uwezo wa kupokea jumla ya takribani lita Bilioni 1.31 mafuta aina ya Petroli,dizeli, mafuta ya Taa pamoja na mafuta ya Ndege kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara" ameeleza Erasto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live