Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yadhamiria kuzalisha wataalamu wa ngozi

C263F60E E7D4 497C B889 9A8931502F70.jpeg Serikali yadhamiria kuzalisha wataalamu wa ngozi

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imedhamiria kuzalisha wataalamu wa teknolojia ya ngozi kwa kuwapeleka wakufunzi nje ya nchi kwa ajili ya kusomea taaluma hiyo ili kuliwezesha Taifa kuzalisha wahitimu mahiri katika taaluma hiyo.

Akiwa jijini Mwanza waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema Zaidi ya shilingi bilioni 19 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha umahiri wa teknolojia ya Ngozi jijini Mwanza ili kuiwezesha taasisi ya teknolojia ya Dar es salaam DIT kampasi ya Mwanza kuzalisha wataalamu wenye uwezo wa kuajirika na kujiajiri wenyewe

‘Kwahiyo wakati tunawekeza hizo bilioni 19.6 kwa ajili ya ujenzi wa majengo naomba tuongeze kasi ya kuandaa wakufunzi wa kufundisha na kama nilivyokuwa nimesema naombeni msitumie fedha zilizopoza kusomesha watu kwenye taaluma tulizonazo kwa sababu ujuzi wa Ngozi hatuna wataalamu wa kutosha tuelekeze huko tupeleke watu wakasome lether bachelor of arts or fashion and design ‘

Dokta Richard Masika ni mwenyekiti wa baraza la DIT amesema ujenzi wa kituo hicho umeshaanza na unahusisha Majengo mawili ya taaluma pamoja na mabweni mawili huku awamu ya pili ikitarajiwa kuhusisha kiwanda cha mafunzo na uchakataji wa ngozi na bidhaa zake na unategemewa kukamilika ifikapo desemba 2024

‘Baraza na taasisi ya teknolojia Pamoja na wana jumuiya tumedhamiria kufanya kazi na kuisimamia miradi hii kwa weledi kwa ubunifu na uaminifu ili tuhakikishe kwamba thamani ya fedha inakuwepo na kuhakikisha yale yaliyodhamiriwa kufanikishwa kupitia miradi hii yanakuwepo’

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Ilemelela Yusuph Bujiku akatumia fusa hiyo kusema matumaini yake ya kufufuliwa kiwanda cha kuchakata ngozi cha Mwanza Tanneries

‘Maswali mengi ya wananchi ni kiwanda hicho kuanza kufanya kazi tuna Imani na Rais wetu maagizo haya aaaliyatoa n kwa hiyo tuna Imani na watendaji katika kutekeleza yaliyosemwa na Rais kwa kiwanda kuanza kufanya kazi’

 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live