Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yadhamiria kutatua kero ushuru wa Mazao

FB IMG 1722893461325 Serikali yadhamiria kutatua kero ushuru wa Mazao

Tue, 6 Aug 2024 Chanzo: dar24

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amekutana na kufanya kikao na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Morogoro, Wenyeviti wa Halmashauri za Mkoa wa Morogoro na Wakurugenzi wa Halmashauri.

Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, kikilenga kushughulikia kero ya ushuru wa mazao, ili usiathiri wananchi wanaojishughulisha na kilimo kwenye.

Kukutana kwao ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoitoa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Mkutano wa hadhara na wananchi wa Mlimba, Ifakara, Ulanga na Malinyi uliofanyika kwenye Uwanja wa Ccm – Ifakara Agosti 5, 2024.

Chanzo: dar24