Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yabariki wawekezaji kufika Msomera

Matinyi Pic 2bnn Serikali yabariki wawekezaji kufika Msomera

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema wawekezaji wa ndani na nje wana ruhusiwa kuwekeza katika eneo la Msomera ili kuleta maendeleo na kusaidia kuboresha maisha ya wananchi walioamua kwa hiari kuhamia eneo hili.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi ametoa kauli hiyo leo Januari 17, 2024 Kijijini Msomera kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari zaidi ya 60 waliokuwa kwenye ziara maalum ya siku nne kwenye Hifadhi ya Ngorongoro na Msomera kushuhudia zoezi linalofanywa na Serikali la kuwahamisha wananchi kwa hiari kupisha uhifadhi na kuwaboreshea maisha yao.

Matinyi amewahakikishia wawekezaji kuwa wanaruhisiwa kuwekeza kama ambavyo wanafanya katika maeneo mengine kwa kuzingatia sheria za nchi huku pia akiwataka wananchi kuchangamkia fursa hizo baada ya jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali za kukamilisha huduma za kijamii na miundombinu yote muhimu.

"Tayari ujenzi wa nyumba 1000 upo katika hatua mbalimbali kwenye eneo la Msomera na kwamba huduma za ujenzi wa shule za msingi na sekindari, zahanati, eneo la mnada, mabwawa ya kunyweshea mifugo, majosho barabara na umeme unafanyika kwa kasi kubwa" amesema Matinyi.

Wakati huo huo amesema tayari kaya 72 zenye jumla ya watu 500 waliojiandikisha kuhama kwa hiari kutoka Ngorongoro kuja Msomera wanatarajiwa kuagwa kesho katika ofisi za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Katika ziara hiyo waandishi wa Habari iliyoratibiwa na Wizara ya Maliasili kupitia Ngorongoro kwa kushirikiana na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali waandishi walipata fursa ya kutembelelea eneo la makazi ya watu Ngorongoro Kisha Msomera.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live