Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yabainisha korosho iliyonunuliwa hadi sasa

35391 Pic+korosho Serikali yabainisha korosho iliyonunuliwa hadi sasa

Wed, 9 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Tangu Serikali ilipotangaza kununua korosho za wakulima kwa bei ya Sh3,300 kwa kilo moja, hadi leo Jumanne Januari 8, 2019 kiasi cha tani 233,742.473 kimeshakusanywa katika mikoa minne ya Lindi, Pwani, Ruvuma na Mtwara.

Katika kiasi hicho jumla ya tani 203,938.953 kimeshapokelewa katika maghala makuu na tani 29,803.52 bado ziko katika maghala ya vyama vya msingi (Amcos).

Akizungumza na Mwananchi, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema kiasi hicho cha korosho zote ni za daraja la kwanza.

“Korosho ambayo tumeshanunua mpaka sasa hivi ni daraja la kwanza tu natumenunua tani 203,938.953 ambazo tumeshazipokea katika maghala makuu, lakini pia tuna korosho tani 29,803.52 ambayo imenunuliwa katika mikoa hiyo lakini bado iko kwenye vyama vya msingi,” amesema Hasunga.

Akifafanua kimkoa amesema katika mkoa wa Lindi korosho iliyonunuliwa na kupelekwa katika maghala makuu ni tani 53,472.592 na iliyopo katika vyama vya msingi ni tani 8,098.51.

Mkoani Mtwara korosho iliyonunuliwa na imepokelewa katika maghala makuu ni tani 120,884.00 na ambayo bado iko katika vyama vya msingi ni tani 2,481.

“Ruvuma tumeshapokea tani 18,408.443, ambayo bado iko kwenye vyama vya msingi ni tani 7251.29, Pwani ni tani 11,173.918 ambayo bado iko kwenye Amcos ni tani 11,972.72,” amesema Hasunga.



Chanzo: mwananchi.co.tz