Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaatoa hofu wakulima wa mahindi

Waziri Bashe 1140x640.jpeg Serikali yaatoa hofu wakulima wa mahindi

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amewatoa hofu wakulima wa zao la mahindi nchini kutokuwa na hofu kuhusu nchi jirani kuzuia mahindi kuingizwa nchini humo.

Akizungumza katika ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Manyara, Bashe amesema hadi sasa Serikali imenunua mahindi yenye thamani ya bilioni 186 na bilioni 143 zimelipwa ambapo baada ya wiki moja bilioni 43 zitalipwa ili vituo vya kuuza mahindi vifunguliwe tena.

Sambamba na hilo amewaeleza wananchi wasiwe na hofu kuhusu tamko la nchi jirani kwamba wanafunga hawataruhusu mahindi kutoka Tanzania kuingizwa nchini kwao, amesema wananchi wasiwe na wasiwasi kwani Serikali ina uwezo wa kununua mahindi hayo.

“Nawala msipate hofu tamko lililotoka nchi jirani kwamba wanafunga hawataruhusu mahindi yetu yaende kwao, msiwe na wasiwasi Serikali ipo pamoja na ninyi. Wakifunga kwa mwaka wananunuaga tani laki nne tu, sisi hizo tani laki nne kama Serikali ya Mama Samia haiwezi kushindwa kuzinunua, nendeni shambani andaeni kilimo, ruzuku inaendelea kutoka” amesema Bashe

Chanzo: www.tanzaniaweb.live