Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaanza mchakato wa mabadiliko sheria reli ya kati

RELII Serikali yaanza mchakato wa mabadiliko sheria reli ya kati

Sat, 25 Feb 2023 Chanzo: Mwananchi

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete amesema serikali imeanza mchakato wa mabadiliko ya sheria ya reli ya kati ili kuruhusu wawekezaji binafsi kusafirisha mizigo kupitia ndani na nje ya nchi.

Mwakibete amesema hayo jana Ijumaa, Februari 24, 2023 mara baada ya kufanya ziara katika Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) na kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa ikiwepo uboreshwaji wa jengo la abiria ikiwepo kuweka thamani za kisasa za kupumzikia abiria na kukagua mabehewa.

Amesema tayari mchakato huo umepitishwa bungeni kwa mara kwa kwanza kwa sasa kinachofuatia kuanza majadiliano ya kamati na wadau kuchangia mabadiliko ya sheria hizo.

“Duniani kote ili reli zetu zilete tija na ufanisi uliokusudiwa njia za reli zinapaswa kutumika na watu binafsi ili kuongeza fedha vinginevyo serikali haitoweza kufanya yenyewe kila mradi wa uwekezaji" amesema Mwakibete

Amefafanua kuwa lengo la kuruhusu wawekezaji binafsi ni kuleta ushindani ambao utachochoea mapato ya serikali katika usafirishaji wa mizigo kutoka mataifa mbalimbali kupitia mpaka wa Tunduma na kunusuru miundombinu ya barabara zetu kuharibika .

“Utaratibu wa kuruhusu wawekezaji binafsi kusafirisha mizigo kupigia njia za reli ya Tanzania Tazara wameanza na wameona manufaa yake katika kuchochea mapato ya Serikali wahisani wameingia kwa kusarisha shehena za mizigo wa wastani wa tani milioni mbili kwa mwaka mpaka tano," amesema

Mwakibete ametaka shirika hilo kuongeza tija kuvutia wawekezaji wengi zaidi ikiwepo kufanyia maboresho jengo la kupumzikia abiria kwa kuongeza bajeti kwa mwaka wa fedha ujao.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara), Mhandisi Fuad Abdallah amesema katika kuimarisha hali ya usalama wa mizigo inayoingizwa nchini wana mikakati ya kujenga kituo cha ukaguzi katika mpaka wa Tunduma.

“Tayari tunao wawekezaji zaidi ya watatu ambao wanatumia reli yetu kusafirisha shehena za mizigo na katika hilo katika maboresho tutaweka mizani ya upimaji wa mizigo inayoingia nchini ili kujua kiwango kinachoingizwa, ”alisema.

Mfanyabishara wa mbao, Josephat Athon amesema kuna kila sababu kuunga mkono juhudi za Serikali kwani imewatizama kwa jicho la kipekee sekta ya ujenzi na Uchukuzi kwa kuboresha njia za reli.

“Gharama za usafirishaji wa mizigo kutumia njia ya barabara imekuwa kubwa tofauti na usafiri wa reli sasa ni wakati wafanyabishara kutumia fursa hiyo ambayo itasaidia Serikali kupunguza gharama za matengenezo ya barabara nchini.

Chanzo: Mwananchi