Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Misri kuwekeza nchini, ikiwemo kampuni ya uwekezaji na maendeleo ya Cairo inayoshughulika na usimamizi wa kiwanda cha ngozi.
Ametoa kauli hiyo jana Jumanne Julai 9, 2019 alipotembelea kiwanda kikubwa cha ngozi cha Robbiki kilichoko Mkoa wa Sharkianchini Misri, kutumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji hao kuwekeza nchini kutokana na uwepo wa malighafi za kutosha za ngozi.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Julai 10, 2019 na ofisi ya waziri Mkuu inaeleza kuwa akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi Misri, Majaliwa amesema Tanzania ina mifugo mingi inahitaji wawekezaji watakaojenga viwanda vya kuchakata bidhaa mbalimbali zitokanazo na mifugo, ikiwemo ngozi.
Amesema Serikali ya Tanzania imeboresha mazingira ya biashara na uwekezaji pamoja na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Yasser Mohamed Ahmed Al Maghraby amesema kiwanda hicho kinahitaji ngozi kutoka Tanzania.
Awali, Majaliwa alitembelea mradi mkubwa wa mabwawa ya kufugia samaki na mradi wa upanuzi wa awamu ya pili ya mfereji wa Suez Canal,
Pia Soma
- Chakachaka atua tamasha la ZIFF
- Mbu wabadili tabia za kung’ata, wapo waenezao dengue
- Uingereza, Marekani zaingia katika mgogoro