Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania yatangaza neema kwa wakulima wa korosho, mbaazi

70588 Koroshoo+pic

Fri, 9 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Lindi. Serikali ya Tanzania imewaondoa hofu wakulima wa zao la korosho juu ya upatikanaji wa masoko kwa kusema lipo la uhakika na masuala yaliyotokea mwaka 2018 ilikuwa ni kwa masilahi ya kulinda wakulima ili kupata bei inayolingana na hadhi na gharama za uzalishaji.

Pia, imewahakikishia wakulima uhakika wa soko la mbaazi na kwamba mwaka 2019 litakuwa nzuri kwani tayari Serikali imefanya mazungumzo na India hivyo kutakuwa na mabadiliko tofauti na miaka iliyopita.

Akizungumza jana Alhamis Agosti 8,2919, Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba alisema mpaka kufikia jana korosho zote zilizokuwa maghalani tayari zimepata mnunuzi na ndani ya muda mchache maghala yote kuanzia kusini hadi Dar es Salaam yatakuwa matupu.

“Hilo ni kuonyesha tumepata mahitaji makubwa ya mnunuzi ya korosho zetu, mahitaji tuliyoyapata hayakidhiwi na korosho tulizo nazo, ndiyo maana inaonyesha dalili hata korosho za msimu huu zitakuwa na soko kubwa na zitanunuliwa kwa bei stahiki kwa sababu tunajua korosho yetu ni bora lakini wakati wa kuzalisha ndio wazalishaji wakubwa duniani,” alisema Mgumba

Alisema korosho ya Tanzania inauzika na wanaopotosha kwamba korosho inaharibika sio kweli na ziko katika hali nzuri iliyoridhisha wanunuzi na kutoa bei ambayo Serikali imeridhika nayo.

Hata hivyo,  aliwataka wakulima wa mikoa ya kusini kufanya mgawanyo wa kilimo cha mazao mbalimbali kwa sababu yanapishana msimu tofauti na korosho ambayo ikishapandwa mkulima anaweza kuvuna kwa miaka mingi.

Pia Soma

“Lazima tujielekeze na kwenye mazao mengine yatatuongezea kipato, tuongeze juhudi kwenye kilimo cha ufuta soko liko kubwa na nyinyi wenyewe ni mashahidi, tuongeze juhudi katika mbaazi na mwaka huu soko litakuwa nzuri tumeshazungumza na wenzetu wa India wamekubali kununua na soko litafunguka mtaona tofauti na miaka miwili iliyopita,”alisema Mgumba

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa alizitaka taasisi zilizoshiriki maonyesho hayo kuendelea katika maeneo hayo ili kuendelea na uzalishaji wa mbegu bora pamoja na kutoa mafunzo kwa wakulima na wafugaji.

“Nimeona kazi iliyofanywa na wataalamu wetu, mikoa ya Lindi na Mtwara tunataka kazi mlizozionyesha katika maonyesho haya muendelee nazo kwa mwaka mzima, Naliendele, Magereza na JKT wameniambia wataendelea kuwepo,hivyo niwasihi wananchi kutumia fursa hii kupata mbinu za kisayansi, teknolojia na ubunifu kutoka kwa taasisi husika kama ni kilimo, uvuvi au ufugaji kwa maslahi ya kuinua uchumi wao kama mtu mmoja mmoja na Taifa,” alisema Byakanwa

Mtafiti wa kilimo na mkaguzi wa mbegu kutoka taasisi ya kuthibiti ubora wa mbegu (TOSCI), Neema Yohana alisema baadhi ya wakulima wamekuwa wakiuziwa mbegu bandia na kuwaletea mazao yasiyo mazuri huku akiwataka kutumia ofisi hiyo na maonyesho yanayofanyika kujua namna ya kutambua mbegu bora na kuepukana na bandia.

“Mbegu bandia zimekuwepo baadhi ya maeneo kwa wakulima kudanganywa kwa sababu hawafahamu wanatakiwa kununua mbegu kwenye maduka ya watu waliosajiliwa na TOSCI zinakuwa zimethibitishwa ubora na pia zina lebo ya TOSCI na wanaponunua wadai risiti ili kuepukana na mbegu bandia lakini kusaidiwa ikitokea ameuziwa mbegu bandia,” alisema Yohana

Chanzo: mwananchi.co.tz