Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania yataka mashamba makubwa ya tumbaku yapimwe

71113 Mashamba+pic

Tue, 13 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Serikali ya Tanzania imeuagiza uongozi wa mkoa wa Tabora kuhakikisha mashamba makubwa ya tumbaku yanapimwa.

Akizungumza na viongozi wa mkoa wa Tabora leo Jumanne Agosti 13, 2019, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania, Angelina Mabula amesema kwa kutopimwa mashamba hayo ina maana Serikali ya Tanzania inakosa mapato.

"Nautaka uongozi wa mkoa kuhakikisha mashamba hayo yanapimwa kwani kama ni kuiba wameiba vya kutosha," amesema Mabula

Awali, mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amemweleza naibu waziri kuwa migogoro ya ardhi mkoani Tabora imepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na mkoa pamoja na wilaya kwa kushirikiana na ofisi ya Ardhi kanda ya Magharibi.

Ameeleza kuwa maeneo ya shule za Tabora Boys na Tabora Girls kuwa yamevamiwa huku wavamizi wa shule ya Tabora Girls, nyumba zao zikibomolewa na wale wa Tabora Boys bado hawajaondolewa wakisubiri maelekezo ya wizara.

Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Tabora, Eric Komanya amesema ifikapo mwaka 2020 migogoro ya ardhi katika Manispaa ya Tabora itakuwa imetatuliwa kwa asilimia tisini.

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz