Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania yataja sababu kukwama mafuta ya kula bandarini

57678 Mafutapic

Thu, 16 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali ya Tanzania imetaja sababu ya mafuta ya kula kukwama bandarini kwamba ni  waagizaji kutowasilisha nyaraka halisi zinazotakiwa.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Mei 15 na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji wakati akijibu hoja iliyotolewa na Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.

Kamati hiyo ilikuwa ikitoa maoni yake kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya viwanda na biashara kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 

Kamati hiyo imesema kuna mzigo wa mafuta wa tani 1,500 umekwama bandarini kwa zaidi ya miezi saba kutokana na mgogoro wa uamuzi baina ya mamlaka za udhibiti kuhusu vipimo vinavyobainisha aina ya mafuta yaliyoingizwa.

Akijibu hoja hiyo, Dk Kijaji amesema wafanyabiashara hao wanatakiwa kuwasilisha nyaraka halisi kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya Forodha ya Afrika Mashariki.

Amesema sheria hiyo inataka mwagizaji wa mzigo kuwasilisha nyaraka halisi na ndio mwenye jukumu la kuhakikisha anawasilisha nyaraka halisi ya mzigo wake.

Pia Soma

“Ni mwaka jana tu kipindi kama hiki ombwe la mafuta lilitokea tujiulize swali la kwanza kwa nini wana target (lenga) kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani?,” amehoji.

Amesema hicho ni chakula ambacho kililetwa nchini ni lazima kuonyesha kilipotoka kwa nyaraka halisi.

“Sisi tuliopewa mamlaka haya ya kusimamia tunataka wananchi walindwe kwa kila hali na lazima tulisimamie jambo hili.”

“Mafuta hayo yalikuja metriki tani 14,400 na kati ya hayo yapo ambayo hawajafanya declaration hadi leo. Yako bandarini kipi kinafichwa katika hilo?,” amehoji.

Amesema dhamira ya Serikali ni njema kwa hiyo kabla hawajabebwa lazima wafahamu kuwa nini kilichopo kwenye mzigo.

“Yapo mengine wame declare lakini hawajaleta original  documents (nyaraka halisi), hatutatoa bila kuleta original documents, hatuwezi kutoa hadi tuwe tumetekeleza sheria,” amesema.

Amesema lengo ni kujiridhisha kama ni mafuta yaliyosafishwa ama ni mafuta yasiyosafishwa hulipiwa kodi kutoka katika nchi yanapozalishwa .

“Kama walilipia kule watuletee tujue thamani yake ili tuweze kuwapelekea Watanzania. Katika mafuta hayo yapo mengine yameondolewa, mwanzo walisema yatatumika ndani ya nchi lakini wameyaondoa na kuyapeleka nchi jirani lipi linafichwa hapo?” amehoji Dk Kijaji.

Chanzo: mwananchi.co.tz