Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania yasema haizitambui Dola 50 milioni za msaada kutoka Benki ya Dunia

20522 Wizafraaa+pic TanzaniaWeb

Wed, 3 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Benki ya Dunia (WB) ikieleza kusitisha msaada wa Dola 50 milioni kwa Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James amesema hawatambui kuwapo kwa msaada wa aina hiyo.

“Serikali haijawahi kuomba wala kuwa kwenye mchakato wa kukopa Dola 50 milioni kwenda kwenye kazi za Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Mimi kama Katibu Mkuu nasema hatujawahi kuandika barua kuomba hizo fedha,” amesema James alipozungumza na MCL Digital leo jioni Oktoba 2, 2018.

Licha ya maoni hayo, katibu mkuu huyo ameitaka MCL Digital kuzungumza na mkurugenzi mkazi wa WB, Bella Bird kujiridhisha kuhusu maombi ya fedha hizo huku akikiri kuwepo kwa mikopo mingine kutoka benki hiyo inayoendelea kutolewa.

Hata hivyo alipotafutwa msemaji wa benki hiyo, Loy Nabeta amesema majibu yaliyotolewa na benki hiyo yalikuwa yanafafanua hoja za mtandao uliochapisha habari husika.

“Majibu yametoka makao makuu (New York-Marekani). Hatuna cha kuongeza wala kupunguza,” amesema

Soma Zaidi:

Benki ya Dunia yashikilia Sh112 bilioni za msaada ikitaka kuboreshwa sheria ya takwimu

Rais TLS azungumzia Benki ya Dunia kushikilia msaada wa mabilioni ya Tanzania

Chanzo: mwananchi.co.tz