Dodoma. Naibu Waziri wa Fedha, Dk Ashatu Kijaji amesema biashara zinazofunguliwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2018 hadi Aprili 2019 ni 16,252 lakini zimefunguliwa 147,818.
Dk Kijaji ameyasema hayo leo Jumatano Mei 15, 2019 wakati akijibu hoja zilizotolewa na wabunge wakati wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya mbunge wa Busega (CCM), Dk Raphael Chegeni wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Viwanda na Biashara mwaka 2019/2020 kudai Dk Kijaji alidanganya Bunge kuhusu takwimu za biashara ambazo zinafungwa.
Pia, Dk Chegeni amesema kuwa mapato yanayokusanywa nchini yameshuka.
Akijibu jambo hilo leo Dk Kijaji amesema huo ndio ukweli na uhalisia na kuhoji kama biashara zingefungwa wasingeweza kukusanya mapato.
Amesema kama biashara zinafungwa maana yake uchumi unasinzia na kubainisha kuwa Tanzania haijafika hapo.
Pia Soma
- Jumuiya na taasisi za kidini kuhakikiwa Tanzania
- Mbunge CCM amtaka Waziri wa Viwanda kuirejesha Kariakoo ya zamani
Amesema tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani hawajawahi kukusanya mapato ya chini ya Sh1trilioni kwa mwezi.