Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania yasaka soko la mbaazi

63582 Mbaazipic

Thu, 20 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Kutokana na kutokamilika kwa mkataba wa makubaliano kati ya Tanzania na India kuhusu soko la mbaazi, Serikali ya Tanzania inaendelea kutafuta masoko mbadala ambayo mazao jamii ya mikundi yatauzwa ikiwa ni pamoja na kuhamasisha matumizi ya ndani.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi Juni 20, 2019 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya wakati akijibu swali la mbunge wa Liwale (CCM), Zuberi Kuchauka aliyetaka kujua Serikali itatatua tatizo la kukosekana kwa soko la zao hilo na kuongeza thamani ya zao hilo.

Naibu Waziri huyo amesema Machi, 2019 Serikali ilifanya ziara ya kutafuta soko la mazao jamii ya mikunde katika nchi jirani za Malawi, Burundi, Kongo DRC na Zambia.

“Kutokana na ziara hiyo nchi ya Malawi kwa mwaka 2019 imeonesha uhitaji wa tani 7,000 za mbaazi. Taratibu za kuhakikisha oda hiyo inatekelezwa zinaendelea kufanyiwa kazi,” amesema Manyanya

Amesema mkakati uliopo wa Serikali ni kuendelea kuhamasisha uwekezaji wa viwanda vya kukoboa na kuongeza thamani kwa mazao ya jamii ya mikundi nchini.

Amebainisha kampuni ya Mahashree Agro Processing Limited ya India inajenga kiwanda mkoani Morogoro kitakachokuwa na uwezo wa kuchakata na kusindika tani 700,000 za mazao jamii hiyo kwa mwaka.

Pia Soma

Amesema kiwanda hicho kinatarajia kuanza uzalishaji Julai, 2019, “Viwanda vingine vilivyojengwa na vinavyofanya kazi ni pamoja na kiwanda chaQuality Pulse Exporters Ltd cha Dar es Salaam na Samon Agro Export Limited.”

Chanzo: mwananchi.co.tz