Arusha. Serikali ya Tanzania imesema imeridhishwa na mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 414 inayopita Mikoa ya Singida, Manyara, Arusha hadi Namanga.
Mkandarasi huyo, Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP) ZTK ilianza kujenga njia hizo mwaka 2017 na kutarajiwa kumaliza Aprili, 2010.
Ujenzi huo unagharimu zaidi ya Sh600 bilioni, hadi sasa umetekelezwa kwa asilimia 51.
Hayo yameelezwa leo Jumanne Julai 23, 2019 na kamishna wa nishati jadidifu, Innocent Luoga wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili ya kukagua ujenzi huo.
Katika ziara hiyo, amekagua njia ya umeme ya Namanga ,kituo cha kupoozea umeme cha Legur kilichopo halmashauri ya Wilaya ya Arumeru pamoja na njia za kusafirishia umeme zilizopo katika halmashauri ya Babati vijijini.
Amesema hadi sasa wameshasimamisha minara zaidi ya 100 kati ya 384 inayotakiwa.
Pia Soma
- Dk Bashiru asema kuna mtu anataka kuivuruga CCM
- Watano kuongezwa kesi ya kutekwa Mo Dewji
- Majaliwa kufungua mkutano Alat
Mkazi wa kata ya Makuyuni, Peter Mollel ameishukuru Serikali kwa kuwapatia mradi huo, kuomba uharakishwe ili kuleta maendeleo katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa viwanda vidogo.