Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania yapata soko la mahindi, mchele katika nchi saba

63051 Pic+soko

Mon, 17 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema imepata masoko ya mahindi na mchele katika nchi saba na kuwataka wafanyabiashara na wakulima nchini kuchangamkia fursa ya kuuza mazao nje ya nchi.

Imesema masoko hayo yamepatikana katika nchi za Omani, Misri, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia, Burundi na visiwa vya Comoro.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Juni 17, 2019 bungeni jijini Dodoma na naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya wakati akijibu swali la mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka.

Katika swali lake Mwakajoka alitaka kujua ni lini Serikali itatafuta masoko ya uhakika ya ndani na nje kwa wakulima wanaozalisha mazao ya chakula kama mahindi na mpunga.

“Aidha, kupitia Tantrade (Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania) tulipokea maombi ya sekta binafsi kutoka nchi ya Rwanda ya kununua tani 102,000, Burundi (100,000), Zambia (3,000) na Comoro tani 3,000 za mahindi kwa kipindi cha mwaka 2018/2019.”

“Kwa mujibu wa takwimu za mauzo ya nje ya TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) tayari takribani tani 39,218 za mahindi zimeshauzwa,” amesema Manyanya.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz