Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania yaagiza tani 225,000 za mbolea

94774 Mbolea+pic Serikali ya Tanzania yaagiza tani 225,000 za mbolea

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali ya Tanzania imeagiza mbolea ya ziada ya kupandia na kukuzia tani 225,000 ili isambazwe kwa wakulima kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini kuharibu mazao mashambani.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Februari 6, 2020 ma Waziri wa Kilimo nchini, Japheth Hasunga katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Amesema mbolea inayohitajika mwaka 2020 kwa ajili ya kupandia na kukuzia ni tani 586,604, kwamba wamelazimika kutoa kibali kwa waagizaji kuongeza tani nyingine 225,000 ili kufidia zilizosombwa na maji.

“Tumetoa kibali watu kuagiza mbolea za kupandia na kukuzia, kila mtu anayetaka kuagiza mbolea afanye hivyo. Nataka  mbolea ziuzwe kama nguo zinavyouzwa madukani ili mradi ziwe na ubora unaotakiwa, zikidhi mahitaji ya udongo wetu na kwa bei elekezi iliyotolewa na Serikali.”

“Hii inatokana na mvua zinazoendelea kunyesha kuharibu baadhi ya mazao na hivyo kusababisha matumizi ya mbolea kuongezeka maradufu na nawaomba watanzania wajitahidi kutumia mbolea maana hawana utamaduni wa kutumia mbolea kabisa,” amesema Hasunga.

Chanzo: mwananchi.co.tz