Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania kuwalipa wakulima wa korosho Sh100bilioni

58719 PIC+MALIPO

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali imesema ndani ya wiki mbili itawalipa wakulima wanaodai fedha zao katika mauzo ya korosho.

Kauli hiyo imetolewa  leo Jumatatu Mei 20, 2019 na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa bajeti ya Wizara hiyo ya mwaka 2019/2020 ya Sh253bilioni.

Hasunga amesema suala la korosho na madeni yake linamuumiza na wakati mwingine hapati usingizi hivyo ataishauri Benki ya Kilimo ikope ili kulipa madeni yake.

Waziri huyo ambaye ni mbunge wa Vwawa amesema korosho zilinunuliwa kwa Sh722.7bilioni lakini zilizokopwa ni  Sh623.6 bilioni, akisisitiza kuwa korosho zilizopo bado nzima na hakuna mashaka kuhusu soko.

Chanzo: mwananchi.co.tz