Arusha. Serikali ya Tanzania imesema itatumia Kiswahili kama bidhaa katika kufikia azma ya uchumi wa viwanda.
Akizungumza wakati wa kufunga maadhimisho ya Kitaifa ya Kiswahili na Utamaduni leo Jumamosi Septemba 14,2019 jijini Arusha, mgeni rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Stella Manyanya amesema Serikali itasimamia lugha ya Kiswahili kufanikisha azma ya kufikia uchumi wa viwanda.
Amesema Serikali ya awamu ya tano imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kinatumika kwa mawanda mapana kwenye Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika.
"Ninampongeza Rais wetu Dk John Magufuli ameleta msukumo mpya katika kukuza na kuendeleza Kiswahili," amesema Injinia Manyanya.
Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita), Dk Selemani Sewangi amesema maadhimisho ya kitaifa yatakuwa yakifanyika kila mwaka kama ilivyokuwa awali miaka kumi iliyopita.
Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (Bakiza), Dk Mohammed Seif Khatib amesema mabaraza ya Kiswahili yataendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kuenzi muungano wetu.
Pia Soma
- Tanzania, Kenya kuanzisha mfuko kulinda bonde la mto Mara
- MWANANCHI JUKWAA LA FIKRA: Bajeti na uwekezaji hafifu unavyotishia ubora wa elimu
- Mkutano viongozi wa dini kuhusu amani kufanyika Zanzibar
Akizungumza kwa niaba ya vyombo vya habari, Charles Hillary amesema Bakita itumie kanuni zake mpya kutoa mafunzo kila mwezi kwenye vyumba vya habari.
Pia, amesema katika sherehe za kitaifa kumekuwa na nishani zikitolewa kwa makundi mbalimbali lakini ni wakati mwafaka kuanza kutambua mchango wa vyombo vya habari hasa katika kukuza Kiswahili.