Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania kufanya utafiti usambazaji wa umeme vijijini

86101 Pic+umeme Serikali ya Tanzania kufanya utafiti usambazaji wa umeme vijijini

Thu, 28 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali ya Tanzania inafanya utafiti kujua tija iliyopatikana kutokana na usambazaji wa umeme vijijini.

Utafiti huo unafanywa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Akizungumza leo Jumatano Novemba 27, 2019 kaimu mkurugenzi mkuu wa REA,  Amos Maganga amesema utafiti huo utaangalia tija katika huduma za elimu, maji na uchumi.

Amesema  hadi Oktoba, 2019 vijiji 8,000 sawa na asilimia 66 ya vijiji 12,268 vilivyopo nchini vilikuwa vimepatiwa umeme.

Amesema lengo ni ifikapo mwaka 2021 vijiji vyote kuwa na umeme.

" Utafiti huu ni muhimu kujua tija iliyopatikana baada ya kusambaza umeme. Tunawaomba wananchi watoe ushirikiano kwa wadodosaji ili tuweze kukamilisha zoezi hili," amesema Manganga.

">Akimwakilisha mkurugenzi mkuu wa NBS, meneja wa takwimu za kilimo na mifugo , Titus Mwisomba amesema wameshaanza maandalizi ya vitendea kazi ikiwemo dodoso kwa ajili ya ukusanyaji takwimu.

Amesema kazi ya ukusanyaji wa takwimu itachukua mwezi mmoja na matokeo yatatolewa Januari, 2020.

Chanzo: mwananchi.co.tz