Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania, Uganda zashauriwa kuboresha mazingira ya biashara

74503 Biasharapic

Sat, 7 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi za sekta binafsi za Tanzania na Uganda zimezitaka serikali za nchi hizo kuboresha mazingira ya biashara ili kuongeza kasi ya ufanyaji wa biashara.

Hayo yamebainishwa na viongozi wa taasisi hizo leo Ijumaa Septemba 6, 2019 katika kongamano la biashara lililowakutanisha wafanyabiashara wa Uganda na Tanzania pamoja na marais wa mataifa hayo, John Magufuli na  Yoweri Museveni.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Salum Shamte amesema Tanzania na Uganda zimekuwa zikifanya biashara kwa muda mrefu lakini biashara hiyo inaweza kuongezeka zaidi ya sasa.

Amesema Serikali inachukua hatua mbalimbali kuboresha mazingira ya biashara na wao wanashirikishwa kikamilifu.

Amezitaka Serikali za nchi hizo kuendelea na uboreshaji wa mazingira ya biashara kwa sababu bado changamoto zipo.

“Tunaomba muendelee kuboresha mazingira ya biashara na kutuhusisha kwenye miradi mikubwa kama ule wa bomba la mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga. Tunaahidi kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo,” amesema Shamte.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Kwa upande wake, mjumbe wa bodi ya sekta binafsi ya Uganda, Mariana Sabune amesema biashara kati ya nchi hizo mbili inakabiliwa na changamoto ya vikwazo visivyo vya kikodi ambavyo vimeweka na nchi husika.

Amesema vikwazo hivyo vimekuwa vikitatiza shughuli za biashara baina ya Tanzania na Uganda na endapo vikwazo hivyo vitaondolewa, wafanyabiashara watafanya shughuli zao kwa ukamilifu bila vikwazo vyovyote.

“Nampongeza Rais Magufuli kwa kuibadilisha sheria ya udhibiti wa chakula na dawa (TFDA), tunaamini kwamba mabadiliko hayo yataondoa vikwazo visivyo vya kikodi,” amesema Sebune kwa niaba ya mwenyekiti wa taasisi hiyo.

Amependekeza makubaliano ambayo yanafikiwa kwenye mikutano ya tume ya pamoja ya kudumu na sekta binafsi yawe yanafanyiwa kazi na kufuatiliwa kwa sababu wamekuwa wakifanya mikutano mingi lakini hakuna utekelezaji wowote.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz