Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania: Hatuwezi kubangua korosho yote nchini

Tue, 26 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema Serikali imefanya tathmini na kubaini uwezo wa viwanda vya ndani kubangua korosho ni tani 50,000 kati ya 222,000 zilizonunuliwa kwa wakulima.

Hasunga ameyasema hayo leo Jumanne Februari 26, 2019 alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa uwezo wa viwanda vya Serikali na binafsi vinaweza kubangua tani 42,000 na Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogovidogo (Sido) ni tani 7,000.

“Tulikuwa tunataka tubangue korosho yote ile nchini, ila baada ya kufanya tathmini na kuangalia uwezo wa viwanda vyetu, tumegundua viwanda vyetu haviwezi kubangua uwezo bado ni mdogo,” amesema Hasunga.

Hasunga amesema Serikali haiwezi kujenga viwanda kwa haraka ili kubangua korosho hizo zitakazosalia ambazo ni tani 172,000 zitauzwa kwa wafanyabiashara na watu wote wa ndani na nje.

“Hawaruhusiwi kwenda kununua kwa mkulima, wananunua kwa taasisi ya Serikali iliyonunua maana tushanunua zote, mnanunua Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko,” amesema Hasunga.

Soma zaidi:  Hasunga aeleza mpango Serikali ya Tanzania kununua ndege ya mizigo



Chanzo: mwananchi.co.tz