Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali, wadau kuendelea kuwainua wananwake kiuchumi

Wananwake Uchumii Uchumiii Uchumii (600 X 341) Serikali, wadau kuendelea kuwainua wananwake kiuchumi

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali itaendelea kushirikiana na wadau ili kuhakikisha wanawake wanapata fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi na kuendeleza biashara zao.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima alipokuwa akizindua Programu ya kuwawezesha wanawake kiuchumi ijulikanayo kama Women Empowerment Program (WEP) inayosimamiwa na kuratibiwa na Benki ya EXIM Tanzania, katika hafla iliyofanyika Agosti 28, 2023 jijini Dar Es Salaam.

Waziri Dkt. Gwajima amesema uchumi unapoimarika ndivyo familia inakuwa na ustawi bora na kupunguza madhira ya vitendo vya ukatili kwenye familia.

“Kwa takwimu tulizonazo, takriban asilimia 70 ya wanawake bado wapo kwenye ajira zisizo rasmi wakijishughulisha na biashara ndogo ndogo kama mama ntilie na kazi za nyumbani. Kwa mfano, kwa mujibu wa takwimu za Finscope za mwaka 2017, kati ya watu 3,014,106 waliokuwa kwenye ajira rasmi, wanawake walikuwa 1,107,917 sawa na asilimia 36.8 tu.” Alisema Waziri Dkt. Gwajima

“Ni matumaini yangu kuwa programu hii ya WEP ya Benki ya Exim imekuja muda muafaka na itakuwa chachu ya kupunguza pengo ili na kuwafanya wanawake washiriki kikamilifu katika sekta ya kifedha” alisisitiza Waziri Dkt. Gwajima

Katika hatua nyingine Waziri Dkt. Gwajima ameipongeza Benki ya Exim Tanzania kupitia mpango huo, kwa kutoa mkopo bila riba wa dola elfu kumi (takribani shilingi milioni 25) kwa wahitimu watatu bora kwa kipindi cha miaka mitatu na kusema jitihada hizo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Jaffari Matundu amesema Benki hiyo imefanikiwa kushirikiana na wadau wengine katika kuwezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa za kupata mikopo isiyo na riba ambayo imewasaidia kupata mitaji na kuongeza vifaa vya uzalishaji hivyo kuongeza masoko kwa ajili ya bidhaa zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live