Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali na ndoto ya kuifufua NARCO

Ranch UFUGAJI MIFUGO Serikali na ndoto ya kuifufua NARCO

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan imeiwezesha Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kiasi cha Shilingi bilioni 4.65 kwa ajili ya kununua vitendea kazi na ng'ombe wazazi ili kuboresha na kuongeza uzalishaji wa kampuni hiyo.

Hayo yamefahamika wakati wa ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega aliyoifanya katika Ranchi ya Kongwa iliyopo Wilayani Kongwa, jijini Dodoma Aprili 27, 2023.

Wakati akizindua matreka mapya matano (5) na kupokea ngo'mbe elfu moja (1000) kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa kampuni ya NARCO, Mhe. Ulega alimshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha kampuni hiyo ili iweze kujiendesha kibiashara.

Alisema lengo la Rais, Dkt. Samia ni kuiimarisha NARCO kwa kuboresha miundombinu na vitendea kazi ili waweze kunenepesha ng'ombe, kuimarisha biashara ya nyama bora ya Kongwa Beef na kuzalisha malisho ya mifugo kwa wingi na kuyauza ndani na nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live