Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali na mkakati kuwainua wavuvi

PICWAVUVI?fit=595%2C300 Serikali na mkakati kuwainua wavuvi

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuwainua wavuvi kwa kuwawezesha vifaa vya kisasa vya uvuvi ikiwemo maboti na vizimba ili waweze kuboresha maisha yao.

Waziri Ulega ameyasema hayo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa vizimba na boti leo Oktoba 3, 2023 jijini Mwanza.

"Mradi huu wa ugawaji wa maboti na vizimba kwa wavuvi bila riba ni wa kwanza, haujawahi kufanywa na yeyote, Rais Dk. Samia ndio wa kwanza kuutekeleza, ametoa jumla ya shilingi bilioni 25 kwa ajili ya kuwezesha wavuvi kupata vifaa vya kisasa ili kuboresha maisha yao", amesema Ulega

Ameongeza kwa kusema kuwa Rais Dk. Samia anafanya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kwa vitendo na hivi karibuni atagawa kwa wavuvi wa Kanda ya Ziwa boti 55 na vizimba 615.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live