Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali mbioni kuwakopesha wafugaji, wavuvi

Mifugo Ya Ngombe 620x308 Serikali mbioni kuwakopesha wafugaji, wavuvi

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema ndani ya Wizara wanafanya utaratibu wa jinsi ya kuwasaidia wafugaji waweze kukopesheka kwa kutumia dhamana zao ili kuwapunguzia manung’uniko.

Ulega ametoa kauli hiyo leo Oktoba 2, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya mkutano huo uliofanyika mwanzoni mwa Setemba mwaka huu.

Waziri amesema katika mkutano huo, wadau 549 walizungumzia sekta ya mifugo moja kwa moja na kubainisha mapungufu kwa ajili ya kuyafanyia kazi ili uwasaidia wafugaji.

Ametaja Wizara hiyo kupata ahadi ya Dola 500 milioni kwa ajili ya mifugo na uvuvi ambazo zitaingizwa kwa awamu, huku akisema kuwa kiasi hicho ni kikubwa lazima kitatoa mwelekeo mpya kwa wafugaji na uvuvi.

“Tulizungumza kwa mawanda mapana, kuna wafugaji wanakuwa na mali nyingi au wavuvi lakini wakopeshaji wanataka dhama za majumba jambo linalowakwamisha watu wetu, hilo tunakwenda kulimaliza sasa,” amesema Ulega.

Wizara hiyo pia imetaja mafanikio mengine kupitia mkutano huo ni kuweka mazingira ya ukopeshaji kwa wafugaji na wavuvi wadogo na uanzishaji wa programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT) kama ilivyo kwa Wizara ya Kilimo.

Kwa mujibu wa waziri huyo, mikoa watakayoanza nayo kwenye BBT ni Tabora, Arusha, Morogoro, Mtwara na Pwani pia tayari maeneo hayo vijana wamejitokeza kwa wingi huku aitaja kuwa watawachukua waliohitimu mafunzo ya JKT, wasomi na makundi mengine ili kupunguza au kumaliza migogoro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live