Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali mbioni kutambua madini yote nchini

MADINI Tanza Madini ya Tanzanite

Wed, 2 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ipo kwenye hatua ya kutambua aina ya Madini yote yanayochimbwa nchini katika maeneo mbalimbali pamoja na kubaini maeneo mapya yenye madini ili Serikali inufaike.

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameyasema hayo alipotembelea machimbo ya migodi ya Vito (Ruby) katika Kata ya Mundarara wilayani Longido Mkoa wa Arusha.

Alisema taasisi zipo mbili, GST hupima juu ya Ardhi na kubaini madini yaliyopo pamoja na STAMICO wanaofanya tafiti za nadini kwa kwenda chini zaidi.

Naye, Kamishina wa Madini Dkt Abdulrahman Mwanga amesema miradi ya kimkakati ni muhimu ili wananchi waweze kunufaika na huduma za kijamii, hivyo amewataka wawekezaji hao kujitahidi kushirikiana na wananchi katika kutekeleza miradi mbalimbali.

"Wawekezaji wanapaswa kutekeleza wajibu na matakwa ya Sheria katika kuendeleza maeneo yao ili kupunguza migogoro inayojitokeza na Wananchi"alisema Dkt Mwanga

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Nurudin Babu aliwaasa wachimbaji hao kufanya kazi kwa kushirikiana na kuepuka mikwaruzano,na matatizo yatakayojitokeza ni vyema yakatolewa taarifa kwake kabla hayajafika kwa Naibu Waziri.

Ofisa Madini Mkoa wa Arusha, Mhandisi Alphonce Rikulamchu amesema uwepo wa madini aina mbalimbali katika wilaya ya Longido ni fursa kubwa ya kiuchumi kwa wakazi wa wilaya na Watanzania wote kwa ujumla.

Mhandidsi Rikulamchu ametoa wito kwa wachimbaji , wafanyabiashara ya madini na wadau wote kuendelea kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu ili kuongeza tija na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato stahiki ya Serikali.

Mmiliki wa kampuni ya Sendeu Agrovet Co. Ltd inayomilikiwa na mwekezaji mzawa Gabriel Sendeu alisema kazi ya uzalishaji inaendelea katika mgodi huo na kueleza kuwa mgodi huu kwa Sasa ni kitovu cha mapato ya Serikali.

" Kampuni yetu imekua ikisaidia miaka yote kusomesha watoto yatima, hii ni baraka naomba na wengine wenye uwezo tusaidie watoto hao waliopo ndani ya jamii", alidai Sendeu.

Alisema kuwa hadi sasa kampuni yao imeweza kuchangia vyema pato la taifa ambapo wameshaweza kulipia tozo mbalimbali huku alibainisha kuwa wameshalipa zaidi ya milioni miatano huku mamlaka ya mapato wakiwa wamepatiwa milioni 350

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha wanamalizia tatizo la ajira hapa nchini wameweza kuajiri jumla ya wafanyakazi wa zawa zaidi ya 100ambao wote wanafanya kazi mgodini apo na wanapatiwa staiki zao zote

Aliomba serikali kuendelea kutatua matatizo ya mipaka ya migodi kwani kumekuwa na shida ya wachimbaji wa migodi hiyo kuingiliana kutokana na kutokujua mipaka yao .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live