Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuzalisha ujuzi sekta ya gesi, mafuta

Gesi Urusii.jpeg Serikali kuzalisha ujuzi sekta ya gesi, mafuta

Sat, 11 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nishati, January Makamba leo Jumamosi Juni 11, 2022 mjini Dodoma wakati wa kutia saini makubaliano ya awali katika Mkataba Hodhi (HGA), kati ya Serikali na Kampuni za Shell na Equinor.

Kilichosainiwa ni baadhi ya vipengere vinavyoweka msingi katika maandalizi ya HGA ambayo bado yanaendelea ili kutoa mwelekeo wa utekelezaji wa Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG).

Msingi wa HGA ndio itazalisha mikataba mingine inayohusisha matumizi ya ardhi, usindikaji, usafirishaji, mauzo ya gesi ya Kimiminika, mauzo ya gesi itakayotumika nchini, matumizi ya bandari, makubaliano ya tozo na mgawanyo wa mapato.

 “Wizara tumejipanga kuhakikisha Watanzania wanashiriki zaidi lakini pia kujenga uwezo wa rasilimali watu ili kuhudumia, kushiriki na kupata manufaa kutoka kwenye mradi,”amesema Makamba.

“Kwa maana hiyo kwa maelekezo yako (Rais Samia Suluhu Hassan) tumeamua tujenge chuo kikubwa cha ufundi polytechnic mahususi kule Lindi kwa ajili ya mafuta na gesi na umeme pia kama sehemu ya kutoa nguvu kazi ya mradi huu na kujenga uwezo wa watanzania.” Amesema Makamba

Chanzo: www.tanzaniaweb.live