Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuwekeza teknolojia sekta ya madini

Wanaharakati Wayataka Makampuni Ya Madini Kuwalipa Zaidi Wachimbaji DRC Haja kubwa kupima TB

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI kuwekeza katika teknolojia ya hali ya juu ya tafiti ili kusaidia kupata taarifa za kijiolojia zitakazowezesha kupata taarifa za kina katika sekta ya madini nchini.

Hali hiyo itafanya kushawishi uwekezaji utakaoongeza ufunguzi wa migodi mingi itakayotengeneza ajira nyingi nchini.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 25, 2023 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, aliyemuwakilisha katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).

Serikali imewataka wadau sekta ya madini kuwekeza katika uchenjuaji, utafutaji, uhifadhi na ufanyaji biashara ya madini kwa kuangalia maslahi ya nchi na watu wake.

Aidha serikali imesema imejipanga kuiwezesha migodi nchini sambamba na wachimbaji wadogo ikiwemo katika upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa kuiunganishia na gridi ya umeme ya taifa.

“Migodi zaidi ya 350 imeunganishwa na gridi ya taifa ya umeme,” amesema Biteko kwa niaba ya Rais Samia.

Aidha amesema serikali imesema itanunua mitambo mingi ili kusaidia wachimbaji wadogo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live