Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuweka nguvu ujenzi wa Makao Makuu ya Posta Afrika

Posta Jengo Jengo la Umoja wa Posta (PAPU) jijini Arusha.

Thu, 2 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dr. Faustine Ndugulile ameshuhudia usimikwaji wa Viongozi wapya wa Shirika la posta Afrika ambapo pamoja na hilo ametembelea ujenzi wa Makao Makuu ya shirika hilo linalojengwa Arusha linalotarajiwa kukamilika June 2022.

Waziri huyo amesema kuwa Umoja wa Posta katika bara la Afrika upo nchini Tanzania, hivyo kama serikali wameweka nguvu katika kuhakikisha ujenzi wa jengo hilo unafikiwa kwa viwango thabiti.

"Umoja wa posta barani Afrika upo Tanzania na hii ni kazi iliasisiwa na hayati Mwalimu Nyerere na sasa hivi tunajenga jengo la kisasa na litakuwa refu zaidi Arusha na lina ghorofa 18 na sisi kama Serikali ya Tanzania tumeweka mchango wetu katika hili jengo- Waziri Ndugulile.

Hata hivyo jengo Hilo la kisasa litajumuisha nafasi maalumu kwa ajili ya shughuli za kitalii,na wananchi ili kujionea vivutio mbalimbali ikiwemo mlima wa Kilimanjaro unaopatika Nchini Tanzania, hivyo unatarajiwa kuongeza na kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live