Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kuwalinda wamiliki wa viwanda

5d56f2064e7d087847e710173cb1af17 Serikali kuwalinda wamiliki wa viwanda

Sun, 19 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuwalinda wamiliki wa viwanda nchini na kwamba haitavumilia kuona wawekezaji wakinyanyaswa.

Majaliwa ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Wananchi baada ya kukagua kiwanda cha kuchakata kahawa cha Ngara Coffee kilichopo wilayani Ngara, Kagera.

Amesema Rais Samia amewaagiza wasaidizi wake wasimamie mwenendo mzima wa masoko ya mazao mbalimbali nchini likiwemo na zao la Kahawa ili kuhakikisha wakulima wananufaika na kazi wanayoifanya.

Amesema Rais Samia ameendelea kuwahamasisha wawekezaji waje nchini na wawekeze katika sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda ambavyo vitawawezesha wakulima kupata masoko ya uhakika ya mazao yao.

Akizungumzia kuhusu kiwanda hicho, Waziri Mkuu amewasisitiza wananchi wa Ngara watumie fursa ya uwepo wa kiwanda cha Ngara Coffee kwa kuongeza ukubwa wa mashamba ya kahawa na soko la uhakika.

Waziri Mkuu amesema uzalishaji wa kahawa kwa wilaya ya Ngara ni tani 1,000 kwa mwaka kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na uwezo wa kiwanda hicho, hivyo amewashauri wakulima waongeza uzalishali ili kukiwezesha kiwanda hicho kupata malighafi ya kutosha.

Aidha, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali, Charles Mbuge aunde timu maalumu itakayofanya mapitio ya mfumo mzima wa uuzaji wa zao la kahawa wilayani Ngara.

Ametoa agizo hilo baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa uuzaji wa zao hilo unaosimamiwa na Chama cha Msingi cha Wakulima wa Kahawa Ngara ambacho kimekuwa kikiwakata wakulima makato mengi na kuwapunguzia tija.

“Makato mengi mnayowakata wakulima hayana msingi kwa mkulima, mfano wa makato hayo ambayo yanakatwa katika kila kilo moja ya kahawa ya mkulima ni pamoja na riba ya mkopo unaokopwa na chama hicho (36%), usafirishaji (34%), gharama za ukoboaji (shilingi 112), gharama ya usafirishaji nje (1%).”

Chanzo: www.habarileo.co.tz