Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kutumia trilioni 36.25 mwaka 2021/2022

B70624c129c4c8b09a51c6f6df0c3985 Serikali kutumia trilioni 36.25 mwaka 2021/2022

Fri, 12 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali nchini inategemea kukusanya na kutumia kiasi cha Shilingi trilioni 36.25 katika mwaka wa fedha 2021/22 ikiwa ni ongezeko la takribani trilioni 1.5 katika kipindi kinachoishia mwezi June mwaka huu.

Akizungumza leo mbele ya Kamati ya Bunge mjini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip amesema fedha hizo zitatoka katika vyanzo vya ndani vya mapato ikiwemo, mikopo yenye masharti nafuu na misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo.

Akiwasilisha mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Kiwango cha ukomo wa bajeti ya Serikali kwa 2021/2022, Dk. Mpango amesema ukomo wa bajeti hiyo unajumuisha mapato ya ndani ya Shilingi trilioni 26.03 ya bajeti nzima.

“Misaada na Mikopo nafuu kutoka washirika wa maendeleo inatarajiwa kuwa takribani Shilingi trilioni 2.88 na mikopo ya ndani na nje itafikia trilioni 7.34.”amesema Dk Mpango

Aidha, ameongeza kuwa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 ni wa kwanza katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka mitano 2021/22-2025/26 wenye dhima ya kujenga uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya watu.

Amesema kuwa mpango huo utalenga utekelezaji wa miradi ya Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere MW 2115, Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa, Makaa ya Mawe-Mchuchuma na Chuma- Liganga na ujenzi wa reli SGR kutoka Mtwara hadi Mbambay na matawi ya Mchuchuma na Kiganga.

Mpango huo pia utatekeleza ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania), Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) – Lindi.

Miradi mingine ni ule wa Kufua Umeme wa Maji - Ruhudji MW 358; Mradi wa Kufua Umeme wa Maji - Rumakali MW 222; Uchimbaji wa madini ya Nickel; Ujenzi wa Madaraja Makubwa na Barabara za Juu za Daraja la Kigongo - Busisi (Mwanza), Tanzanite (Dar es Salaam) na Interchange ya Kamata (Dar es Salaam).

Chanzo: www.habarileo.co.tz