Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kutumia Bilioni 4.6 kuibadilisha Ranchi ya Kongwa

Group Of Cows In A Field Scott E Barbour Serikali kutumia Bilioni 4.6 kuibadilisha Ranchi ya Kongwa

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: dar24.com

Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 4.6 kwa ajili ya kufanya maboresho makubwa katika ranchi ya Kongwa ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mbegu bora za ng’ombe, uchimbaji wa visima na ununuzi wa matrekta.

Hayo yameainishwa na Meneja wa Ranchi ya Kongwa, Elisa Binamungu wakati akisoma taarifa ya utendaji wa shamba la mifugo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua shamba la mifugo la NARCO – Kongwa ili kujionea maendeleo ya shamba na shughuli za ufugaji.

Amesema Serikali imeongeza uzalishaji wa nyama ya ng’ombe, ambapo ranchi ina ukubwa wa hekta 38,000 zenye uwezo wa kuweka uniti za mifugo 25,000 na kwamba eneo la Kongwa lipo kimkakati hivyo menejimenti ya shamba hilo itumie fursa hiyo kuuza bidhaa zake na kujitangaza ili waweze kunufaika na uwepo wa barabara kuu..

“Eneo hili limegawanywa katika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza ina jumla ya uniti za mifugo 12,427 na sehemu ya pili ina uniti za mifugo 16,897 na sisi tuna mifugo mingi sana ila mazao haya ya mifugo na nyama hayauziki nje kwa kiasi kikubwa,” amesema Binamungu.

Chanzo: dar24.com