Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kutoa uamuzi kitalu C baada ya wiki mbili

Tanzanite Pic Data Serikali kutoa uamuzi kitalu C baada ya wiki mbili

Wed, 26 Jan 2022 Chanzo: mwananchidigital

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahidi kutoa tamko baada ya wiki mbili juu ya matumizi ya kitalu C cha machimbo ya madini ya Tanzanite ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambacho kimesimama kufanya kazi kwa zaidi ya miaka minne.

 Waziri Mkuu Majaliwa ametoa ahadi hiyo leo Jumatano Januari 26, 2022 baada ya kukagua soko la madini ya Tanzanite na kutembelea eneo la EPZA lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa maduka na viwanda vya kuongeza thamanin madini hayo.

Amesema baada ya wiki mbili Serikali itatoa uamuzi juu ya kitalu C ambacho kwa muda wa zaidi ya miaka mine kimesimama kufanya kazi.

“Tutafanya tathimini juu ya madeni ya kampuni iliyokuwa wamiliki awali, mali zilizopo ndani ya kitalu hicho na baada ya wiki mbili kutoka sasa tutakuja na majibu juu ya eneo hilo,” amesema.

Awali, kitalu C kilikuwa kinamilikiwa kwa ubia na kampuni ya Sky Group Associates kupitia TanzaniteOne kwa asilimia 50 na Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kwa asilimia 50.

Ofisa madini mkazi wa madini Mirerani, Fabian Mshai amesema tangu kuanzishwa kwa soko la madini Mirerani Julai 2021 hadi Januari 2022 wametoa vibali 105 vya kusafirisha  nje ya nchi.

Mshai amesema madini hayo yamesafirishwa kwenye nchi za India, Ujerumani, China, Marekani, Thailand, Uingereza, Hispania na Uswisi.

Amesema kiasi cha kareti 15,820.51 za madini ya Tanzanite yaliyoongezwa thamani yenye thamani ya Sh2.6 bilioni yalisafirishwa nje ya nchi na Serikali kupata Sh52.7 milioni.

“Pia madini ghafi ya Tanzanite ya kilogramu 10,004.02 yenye thamani ya Sh3.8 bilioni yalisafirishwa kwenda nje na Serikali kuingiza kodi ya Sh270 milioni na Halmashauri ya Simanjiro Sh16 milioni,” amesema Mshai.  

Chanzo: mwananchidigital